Mnamo tarehe 5 Oktoba, Balozi wa China katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, alikutana na Katibu Mkuu wa EAC, Mhe. Stephen Mbundi, jijini Arusha, Tanzania, na baadaye wakafanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Balozi Chen aliipongeza EAC kwa mafanikio yake katika kuendeleza mchakato wa ujumuishaji wa kikanda, huku akieleza kuridhishwa na uhusiano kati ya China na EAC. Pia alifafanua msimamo wa China kuhusu suala la Taiwan na kueleza maudhui makuu pamoja na umuhimu wa GDI (Mpango wa Maendeleo Duniani) katika ngazi ya kimataifa.

Katibu Mkuu Mbundi alisisitiza dhamira ya EAC ya kuzingatia Kanuni ya China Moja, na kupongeza mchango wa Mpango wa Maendeleo Duniani (GDI) katika kuendeleza maendeleo duniani.