Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Mahojiano ya Balozi Chen Mingjian katika kipindi cha “Maelfu ya Maili kwenye Barabara ya Hariri · Rangi za Afrika”, sehemu ya “Mazungumzo na Mabalozi”
2026-08-28 16:24

Mnamo tarehe 17 Agosti, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, alifanya mahojiano katika Ubalozi wa China na kipindi cha “Mazungumzo na Mabalozi”, sehemu ya programu ya “Maelfu ya Maili kwenye Barabara ya Hariri · Rangi za Afrika”, inayotayarishwa na Kundi la Muunganiko wa Vyombo vya Habari la Redio na Televisheni la Shaanxi chini ya mfumo wa Mwaka wa 2026 wa China na Afrika wa Mabadilishano ya Watu kwa Watu.

Balozi Chen alifafanua fursa na mafanikio yaliyotokana na sera ya China ya kutotoza ushuru wa forodha (zero tariff), ambayo imechangia kufungua uwezo mkubwa wa uchumi wa Tanzania. Pia alieleza matarajio makubwa ya kufufua na kuboresha Reli ya TAZARA, ili iwe njia ya maendeleo na ustawi kwa wananchi.

Aidha, alibainisha kuwa kuandaliwa kwa Mwaka wa 2026 wa China na Afrika wa Mabadilishano ya Watu kwa Watu, sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika, ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya Rais wa China, Mhe. Xi Jinping, na viongozi wa Afrika. Alisema hatua hiyo itatoa msukumo mpya katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya wananchi wa China na Afrika.

Baada ya mahojiano hayo, Balozi Chen aliweka rasmi muhuri kwenye kadi maalum ya kumbukumbu ya safari ya timu hiyo barani Afrika, akiihimiza timu hiyo kuwa daraja la vyombo vya habari katika kuendeleza urafiki wa jadi na kusimulia kwa uhalisia hadithi za China na Afrika zinazosonga mbele pamoja kwa ushirikiano katika zama mpya.

Suggset To Friend:   
Print