Balozi Chen Mingjian Akutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu
2026-06-12 16:41
Mnamo tarehe 26 Mei, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, alikutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, mjini Dodoma.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili kati ya China na Tanzania na kusisitiza tena dhamira yao ya kuendelea kuunga mkono na kutekeleza Sera ya China Moja.