Balozi Chen Mingjian Akutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania
2026-06-12 16:41
Mnamo tarehe 26 Mei, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, alikutana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, mjini Dodoma.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya Tanzania na China, hususan katika sekta za mifugo na uvuvi.