Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Balozi Chen Mingjian Ahudhuria Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Uendeshaji wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari ya Chapa ya HOWO cha Saturn Corporation Limited
2026-06-12 16:38

Mnamo tarehe 24 Mei, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Mhe. Judith Kapinga, walihudhuria maadhimisho ya miaka miwili ya uendeshaji wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari ya Chapa ya HOWO cha Kampuni ya Saturn Corporation Limited na kuzindua rasmi awamu ya pili ya mradi huo.

Mshauri wa Ubalozi wa China, Bw. Chu Kun, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri, pia walihudhuria hafla hiyo.


Suggset To Friend:   
Print