Tarehe 23 Mei, Balozi wa China nchini Tanzania, Mheshimiwa Chen Mingjian, pamoja na watumishi wa Ubalozi wa China, walishiriki Mbio za Afrika Day Marathon 2026, zilizoandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania pamoja na Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Paul Christian Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Mkuu wa Mabalozi (Dean of the Diplomatic Corps) nchini Tanzania, mabalozi, wanadiplomasia pamoja na zaidi ya wananchi 1,000 walishiriki katika tukio hilo.
Balozi Chen alibadilishana mawazo na mawaziri hao wawili kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja.