Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, alitoa hotuba yenye mada kuhusu“Sera ya Mambo ya Nje ya China” katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania tarehe 10 Aprili. Hotuba hiyo ulihudhuriwa pia na Afisa wa Ulinzi wa Ubalozi wa China, Kanali Mwandamizi Wang Haijun.
Balozi Chen alifafanua kwa kina kuhusu diplomasia ya China kama taifa kubwa yenye sifa za Kichina, ikiwemo juhudi za kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa wanadamu, kuandika kwa pamoja sura mpya ya jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja wa kila hali katika enzi mpya, pamoja na kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya China na Tanzania. Aidha, alijibu maswali mbalimbali ikiwemo kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani.
Balozi Chen alikutana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Meja Jenerali Wilbert Augustin Ibuge, kabla ya hotuba hiyo.

