Mwanzo > Maelezo kuhusu ubalozi wa China > Risala ya balozi
Ujumbe wa Balozi
2023-04-18 16:31

Karibu kwenye tovuti ya Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Tanzania ni nchi nzuri yenye mazao mengi, na watu wa Tanzania ni marafiki, wakarimu, waaminifu na wenye imani ya matumaini mema. Kwa miaka mingi, Tanzania inadumisha uimara wa muda mrefu na maendeleo mapya yaliyopatikana moja baada ya mengine katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tanzania imekuwa nchi yenye ushawishi mkubwa katika Afrika mashariki na kusini.

Ukijengwa na viongozi wa zamani wa kizazi kilichopita wa nchi hizo mbili, urafiki wa China na Tanzania, umekuwa wa karibu zaidi kadiri muda unavyoendelea. Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ni kumbukumbu ya milele katika historia ya uhusiano kati ya China na Afrika. Mwaka 2013, Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kushika wadhifa wa urais, alikuja Tanzania na kupendekeza hapa kwa mara ya kwanza kanuni ya uaminifu, matokeo ya kweli, uhusiano wa kirafiki na nia njema pamoja na kanuni ya kutafuta maslahi mazuri na yenye manufaa kwa wote. Ushirikiano wenye malengo ya pamoja kati ya China na Tanzania umekuwa na matokeo mazuri. China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Tanzania na chanzo kikubwa zaidi cha uwekezaji wa kigeni kwa miaka kadhaa mfululizo. Ubalozi wa China nchini Tanzania utaendelea kufanya jitihada zisizo na kikomo za kukuza urafiki kati ya China na Tanzania na kuinua ushirika wa kina wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kuwa wenye manufaa zaidi. 

Natumai tovuti hii inaweza kutumika kama daraja la kuimarisha urafiki kati ya watu wa China na Tanzania kwa kutoa taarifa za hivi punde kuhusu nchi hizi mbili na uhusiano wa nchi hizo mbili kwa marafiki katika sekta mbalimbali.

Chen Mingjian

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Suggset To Friend:   
Print