Tarehe Mei 14, Balozi wa China nchini Tanzania H.E. Chen Mingjian alifanya mkutano wa waandishi wa habari wenye mada "Azimio Namba 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UM) Halina Pingamizi, na Kanuni ya China Moja Lazima Iteteweke." Vyombo 11 vya habari vya Tanzania na China, ikiwa ni pamoja na The Daily News, The Guardian, Tanzania Broadcasting Corporation, na Shirika la Habari la Xinhua, vilishiriki mkutano huo.
Balozi Chen alielezea muktadha wa kihistoria wa swali la Taiwan na kiini cha Azimio Namba 2758 la Baraza Kuu la UM, na alisisitiza kuwa Taiwan ni sehemu isiyeweza kutenganishwa ya eneo la China kutokana na mtazamo wa kihistoria, kisiasa na kisheria. Alikanusha upotoshaji na changamoto za makusudi kuhusu Azimio hilo kutoka kwa baadhi ya watu nchini Marekani, na alithamini sana msimamo thabiti wa Tanzania wa kufuata kanuni ya China moja. Pia, alitamani kuwa Tanzania itaendelea kukabilia kwa nguvu na aina yoyote ya "Uhuru wa Taiwan", kuunga sana juhudi zote za serikali ya China katika kufikia umoja wa taifa, na kushirikiana katika kulinda matokeo ya ushindi wa Vita Kuu vya Pili vya Kidunia.
Balozi Chen pia alijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.