Hivi karibuni, shindano la "Simulizi Yangu ya China" la Picha na Video la China-Afrika lilizinduliwa rasmi. Hafla hiyo imefadhiliwa na Sekretarieti ya Kamati ya Ufuatiliaji ya China ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Chama cha Diplomasia ya Umma cha China, na kuandaliwa na Global Times Online.
Shindano hilo linatarajiwa kuunganishwa na waandaaji wa maudhui kutoka China na Afrika, wakilenga kuonyesha urafiki kati ya pande hizo mbili katika kipindi cha miongo sita iliyopita kupitia picha, michoro ya rangi na video fupi. Inaangazia hadithi za michezo, utamaduni, uchumi na biashara ya China na Afrika, na kuwaalika wabunifu kutoa mitazamo yao binafsi juu ya China, marafiki wao wa China na uzoefu nchini China, ili kuangazia uhusiano wa karibu kati ya watu wa China na Afrika na matumaini yao kwa maendeleo chanya ya uhusiano kati ya China na Afrika.
Shindano hili limeanza kwa mawasilisho mtandaoni, likiwakaribisha washiriki kujiandikisha kama watu binafsi au kwa niaba ya mashirika. Shindano linachukua mchanganyiko wa upigaji kura na uchambuzi wa kitaalamu. Jamii inaweza kutembelea kurasa za shindano katika kipindi kilichobainishwa kupiga kura. Kazi 150 zenye kura nyingi zaidi zitaendelea hadi awamu ya uchambuzi wa wataalamu, ambapo jopo la wataalamu litathmini kulingana na vigezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubora wa picha, kuonyesha hisia na uwasilishaji wa mtazamo, ili kuamua washindi wa mwisho.
Shindano hilo litatambua washiriki bora wenye tuzo kama vile "Katika Picha Tunaonana - Tuzo ya Picha Bora” na "Ushahidi wa Video - Tuzo ya Filamu Fupi Maarufu". Kila kitengo cha tuzo kinajumuisha tuzo za kwanza, za pili, na tatu, pamoja na tuzo bora. Washindi watapata zawadi za pesa taslimu kuanzia dola 100 hadi 500, cheti cha kielektroniki, pamoja na nafasi ya kualikwa China.
Kipindi cha uwasilishaji wa kazi kinaanza sasa hadi 12:00 PM Mei 10, 2024. Washiriki wanaweza kutuma kazi zao kwa anwani ya barua pepe iliyobainishwa:
videophoto@huanqiu.com. Maelezo zaidi kuhusu shindano hilo yametolewa hapa chini.
Mwongozo kwa washiriki wa Shindano la “Simulizi yangu ya China” la Picha na Video la China-Afrika.
I. Nani anaweza Kushiriki
Waandaaji wote wa maudhui kuhusu China na Afrika wenye dhamira ya kukuza urafiki wa China-Afrika.
II. Lugha
Kichina, Kiingereza, Kifaransa
III. Ratiba ya Shindano (Majira ya Beijing)
Muda wa Kuwasilisha: Kutoka sasa mpaka 12:00 Mei 10, 2024
Upigaji Kura: Kutoka 12:00 Mei 14 mpaka 12:00 Mei 21, 2024
Uchambuzi wa Wataalamu: Kutoka Mei 24 hadi Juni 7, 2024
Kutangaza Matokeo: Juni 2024
IV. Tuzo
Shindano hili linatoa tuzo za "Katika Picha Tunaonana - Tuzo ya Picha Bora” na "Ushahidi wa Video - Tuzo ya Filamu Fupi Maarufu."
Muhimu: Kila kundi la tuzo linajumuisha ya kwanza, ya pili na ya tatu na pia tuzo bora. Washindi watapokea tuzo ya pesa taslimu kuanzia dola 100 mpaka 500, cheti cha kielektroniki na pia fursa ya kwenda China. Kila kazi inaweza kushinda tuzo moja tu.
V. Mahitaji ya Kazi
1. Vigezo vya Wazo
Kazi zinatakiwa kuzingatia wazo la “Simulizi Yangu ya China” ikiwa na kichwa cha habari walichojitengenezea. Maudhui pendekezwa yanajumuisha, lakini si hayo pekee: Niionavyo China (Taswira binafsi kuhusu utambulisho wa miundombinu ya China, filamu na tamthilia n.k.), Wachina marafiki zangu, safari yangu kwenda China, simulizi za China-Afrika (michezo, utamaduni na maeneo mengine), n.k.
2. Mahitaji ya Picha
Picha zinatakiwa kuwa katika mfumo wa jpg/png, na kila faili lisiwe chini ya MB1. Kila kazi lazima iwe na kichwa cha habari, na iambatane na maelezo yasiyozidi maneno 300. Picha moja au mlolongo wa picha (mpaka picha 4 zikiwa na vipimo sawa) zinakubalika, zikiwa na rangi nyeusi, nyeupe au za rangi. Kazi zote zinaweza kupunguzwa ukubwa, lakini haitakiwi kuhariri kazi baada ya uzalishaji na hairuhusiwi kuziunganisha picha kadhaa kwa kutumia kompyuta ili kuleta mvuto zaidi. Hakuna ukomo wa idadi ya kazi za kuwasilishwa na kila mshiriki.
3. Mahitaji ya Video
Kazi lazima ziwe na sura kamili, sauti na vichwa vidogo vya habari (Kichina, Kiingereza au Kifaransa), zisizidi dakika 3, Chinese, English, or French), ziwe na walau ubora wa pixeli 1280*720, na ziwe katika mfumo wa MOV/MP4/AV. Kila kazi lazima iwe na kichwa cha habari ikiambatana na maelezo yasiyozidi maneno 300. Video lazima zioneshe vizuri na zisiwe na alama za mipaka, nembo, chapa au kitambuzi chochote. Matangazo ya video za kibiashara hayaruhusiwi. Hakuna ukomo wa idadi ya kazi zinazowasilishwa na kila mshiriki.
4. Maelezo ya Hakimiliki na Miliki Ubunifu
a. Kazi lazima iendane na wazo la shindano na itoe ujumbe chanya. Maudhui yenye utata, ikiwemo picha za ngono, katili, udini na ubaguzi wa rangi, au ubaguzi wa kikanda, hazitakiwi.
b. Washiriki lazima wathibitishe kuwa wanahaki miliki ya kazi zao. Muandaaji hatohusika na mgogoro wowote wa kisheria au hasara kuhusiana na mgogoro wa haki za umiliki wa picha, haki za heshima, haki za faragha, haki za umiliki na haki za nembo za biashara.
c. Kazi zinaweza kutumika kama nyenzo za matangazo kwa ajili ya shughuli za mawasiliano zenye uhusiano na tulio zisizolenga kupata faida (ikijumuisha lakini si hizi pekee za maonyesho, utangazaji, uchapishaji, uzalishaji wa bidhaa, n.k), pasipo na fidia ya ziada.
d. Washiriki wanatakiwa kuonesha vyanzo vya kazi zao na kuheshimu taratibu hapo juu kabla ya kuingia kwenye shindano ili kukidhi taratibu za shindano.
e. Washindi wa tuzo wanatakiwa kutoa taarifa zao binafsi kwa muandaaji kwa ajili ya kutuma tuzo.
f. Muandaajia anaweza kutoa tafsiri ya mwisho ya kanuni na taratibu za shindano ikiwa ni muhimu.
VI. Namna ya Kushiriki
Washiriki wanatakiwa kutuma mafaili ya kazi zao na fomu ya kushiriki kwenye anwani ya barua pepe ifuatayo: videophoto@huanqiu.com. Barua pepe lazima ijumuishe jina la mtu, utaifa, mwajiri au taasisi shirikishi, namba ya simu, anwani ya barua pepe, na taarifa nyingine vinazoendana.
Washiriki pia wanakaribishwa kuchangia kazi zao kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na hashitagi.
Kwenye jukwaa la Kichina: #我的中国故事# kwa ajili ya majukwaa kama Weibo, AAuto Quicker, Douyin, na bilibili.
Majukwaa ya nje: #MyChineseStory# kwa majukwaa kama Facebook, Twitter, YouTube, and TikTok.
* Muhimu:
1. Ikiwa mshiriki ana kazi nyinyi, tafadhali weka mafaili yote ya picha zote na video na fomu ya ushiriki katika fungu moja.
2. Majina ya faili la utangulizi wa picha/video lazima yaendane na jina lililotajwa katika fomu iliyotumwa. Kwa mfano, ikiwa kazi inaitwa “Change” katika fomu ya ushiriki, zote picha/video asilia na fomu ya taarifa lazima ziitwe “Change.”
3. Baada ya usajili, Kamati ya Maandalizi itawataarifu washirki kuhusu matokeo ya usajili kupitia barua pepe ndani ya siku tano za kazi.
4. Tafadhali angalia fomu ya ushiriki kwa ajili ya taarifa za usajili, au pakua kupitia kiungo kifuatacho:
China (Baidu Netdisk):
Kiungo: https://pan.baidu.com/s/1ykSkSQNOIi1IAHIhpB2eCA
Kodi ya kuingia: 416g
Ughaibuni (Google Drive):
https://drive.google.com/drive/folders/18T6k-ndekYuXI5hfDQQ8ibm9GD7AB462? usp=sharing
Ⅶ. Vigezo vya Tathmini
Shindano litatumia muunganiko wa upigaji kura wa jamii na uchambuzi wa wataalamu kuchagua kazi za mwisho zenye ushindi.
Mbinu maalumu za tathmini ni kama ifuatavyo:
Sehemu 1. Maonyesho
Tovuti maalum itaanzishwa kwa ajili ya kuonyesha kazi, na Muandaaji ataorodhesha kazi ambazo zinakidhi wazo na mahitaji mengine ya shindano.
Sehemu 2. Upigaji kura
Upigaji kura utafunguliwa kwenye tovuti ndani ya muda uliowekwa, na kazi 150 bora zitaingia katika awamu ya uchambuzi wa wataalam.
Phase 3. Ukaguzi wa wataalam.
Kazi zitatathminiwa kulingana na namna picha zilivyochukuliwa na kuwekwa, mawasiliano yenye hisia, na namna mtizamo ulivyoelezwa kabla ya orodha ya kazi zilizoshinda kutolewa.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:
E-mail: videophoto@huanqiu.com
Tel: +86-10-65361101-3002
Kiambatanishi: Fomu ya Ushiriki wa Shindano la “Simulizi yangu ya China” la Picha na Video la China-Afrika.