Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Wanafunzi wa Tanzania Washinda Tuzo ya Kwanza ya Shindano la TEHAMA la Huawei Kusini mwa Jangwa la Sahara
2019-03-15 22:50
Wanafunzi watatu wa Chuo kutoka Tanzania, pamoja na wenzao kutoka Nigeria, walishinda tuzo ya kwanza katika shindano la mwisho la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano la Huawei Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mashindano ya Mwisho ya Kusini mwa Jangwa la Sahara yalifanyika Johannesburg, Afrika Kusini kutoka Machi 8 mpaka 10, 2019.
 

 

Washiriki wa kundi la Tanzania walikaribishwa kwa upendo na wafanyakazi wa Kampuni ya Huawei Tanzania katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Machi 11, 2019

Likisimamiwa na Bw. Oscar Mashauri, mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanafaunzi watatu watanzania ni Bw. Emanuel Lucas Chaula kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bw. Yusuph Hamisi kutoka Chuo Kikuu Huria, na Bw. Joakim Kelvin Ngatunga kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma.

Pamoja na washindi wa tuzo ya pili kutoka Angola na Kenya, makundi hayo manne yatakwenda China mwezi wa tano kwa ajili ya mashindano ya mwisho ya kimataifa yatakayofanyika Shenzhen, mji ambapo ni Makao Makuu ya Huawei. Wakati huo, watashindana na takribani makundi 40 kutoka sehemu nyingine za dunia kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

 

Makundi manne ya washindi wa mashindano Kusini mwa Jangwa la Sahara. Picha imepigwa Johannesburg, Afrika Kusini, Machi 10, 2019.

Ikizinduliwa mwaka 2015, Mashindano ya TEHAMA ya Huawei ni mashindano ya vipaji ya mwaka ya TEHAMA yanayohusu; utunzaji wa taarifa kwenye mtandao (cloud computing), nadharia na maendeleo ya mifumo ya komputa kufanya kazi za binadamu (artificial intelligence), mitandao ya simu (mobile networks) na mkusanyiko mkubwa zaidi wa taarifa zinazoweza kuchambuliwa kwa komputa kuonesha mifumo, mienendo na mahusiano hususani kuhusiana na tabia za binadam na muingiliano (big data). Washiriki wa mashindano walitokana na taarifa zilizothibitishwa na Huawei na Chuo cha Teknolojia za Mitandao (kiitwacho Huawei ICT academies) na vyuo vingine vinavyohusiana na TEHAMA. Tukio la 2018/19 limevutia washiriki 80,000 kutoka nchi zaidi ya 50. Nchi hizi 50 zinagawanywa katika makundi 12 kulingana na maeneo yao ya kijiografia, ikiwa ni pamoja na Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika ya Kaskazini, Ulaya ya Magharibi, Kaskazini na Mashariki mwa Ulaya, Mashariki ya Kati, Eurasia, China, Japan, Asia ya Kusini-Mashariki, Pasifiki ya Kusini, Amerika na Amerika Kusini. Washiriki wanapaswa kushinda shindano katika ngazi za kitaifa na kikanda ili kuendelea na fainali za kimataifa.

Wanafunzi karibu 30,000 kutoka vyuo vikuu zaidi ya 100 nchini Nigeria, Ghana, Kenya, Uganda, Tanzania, Angola, Afrika Kusini, Msumbiji, Zambia, Botswana na Mauritius walishiriki fainali za Kusini mwa Jangwa la Sahara. 

Suggset To Friend:   
Print