Mwanzo > Uhusiano kati ya China na Tanzania > Siasa
Ubalozi wa China na Serikali ya Tanzania ziliandaa kwa pamoja Safari ya Ukumbusho wa TAZARA kwa Vijana
2018-11-09 20:21

Ubalozi wa China na Serikali ya Tanzania ziliandaa kwa pamoja Safari ya Ukumbusho wa TAZARA kwa Vijana

Ili kuendeleza ari ya TAZARA, urithi wa urafiki wa jadi wa China na Tanzania, na kukuza utalii na uhifadhi wa wanyamapori sambamba na reli ya TAZARA, Ubalozi wa Kichina nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mamlaka ya TAZARA, ziliandaa safari ya maadhimisho ya TAZARA kwa vijana wa nchi hizo mbili Novemba 3, 2018.

Sherehe ya Uzinduzi

Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke, Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Mhandisi Timothy Kayani waliungana na wanafunzi wa Vyuo Vikuu, wanadiplomasia vijana wa Ubalozi wa China na Walimu wa Kichina na pia Wachina wakujitolea kutoka Taasaisi ya mafunzo ya Lugha ya Kichina ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakihudhuria tukio hilo. 

Balozi Wang Ke akitoa hotuba yake

Katika hotuba yake kwenye sherehe ya uzinduzi, Balozi Wang Ke alisema kuwa TAZARA sio tu mradi wa mfano unaohusisha urafiki wa China-Afrika na China-Tanzania, lakini pia ni kitabu kizuri cha watu katika nchi hizo mbili, hasa kwa kizazi kidogo, kujifunza historia ya urafiki wa China na Tanzania na kujenga Maisha bora yajayo kwa mahusiano ya nchi mbili. Kwa maoni yake, TAZARA pia inaweza kutumika kama jukwaa muhimu kwa Serikali ya Tanzania ili kukuza ulinzi wa wanyamapori na utalii kwa kuwa inapita maeneo kadhaa ya uhifadhi wa wanyamapori.

Waziri Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba yake

Waziri Hamisi Kigwangalla aliisifia sana TAZARA, "Reli Kuu ya Ukombozi", na kuishukuru Serikali ya China kwa kutoa msaada wa kusaidia shughuli za uhifadhi nchini Tanzania, akitoa mfano wa mchango wa magari 50 maalum kwa kufanya doria katika hifadhi za taifa na mbuga za wanyama katika miaka ya hivi karibuni.

Picha ya Pamoja

Katika Hifadhi ya Taifa ya Selous, Balozi Wang Ke, kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, alitoa msaada wa vifaa vya ofisi na vifaa vya matumizi ya kila siku kwa Mamlaka ya Wanyamapori ya Tanzania (TAWA), ambayo ni shirika la serikali linaloongoza uhifadhi wa wanyamapori katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Selous. Aliwahimiza wadau kutumia kikamilifu TAZARA ili kukuza utalii na maendeleo ya kiuchumi, kugeuza rasilimali nyingi za asili kuwa faida za kiuchumi. 

Balozi Wang Ke akimkabidhi Waziri Hamisi Kigwangalla tarakilishi mpakato

Washiriki wengi vijana hawajawahi kushuhudia safari ya Hifadhi ya Taifa ya Selous kupitia TAZARA. Mbali na furaha na msisimko, safari hiyo imewapa nafasi nzuri ya kujifunza historia ya TAZARA na kuimarisha ufahamu wao juu ya urafiki wa China na Tanzania.

Balozi Wang Ke, mawaziri na wanafunzi wakiimba wimbo pamoja

Balozi Wang Ke akifurahia pamoja na vijana

Suggset To Friend:   
Print