Mwanzo > Habari kuhusu China
Jacqueline Liana: Sera ya China moja zao la historia lililothibitishwa UN
2025-05-27 14:33

Jacqueline Liana, Katibu Msaidizi wa Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania, hivi karibuni alichapisha makala yenye kichwa "Sera ya China moja zao la historia lililothibitishwa UN" katika magazeti mawili ya Tanzania, yaani Uhuru na Guardian. Hapa chini kuna nakala kamili ya makala hiyo.

DUNIANI kuna China Moja tu. Hili ni tamko la kisera na kisheria la Jamhuri ya Watu wa China (PRC). Linatambuliwa na kutekelezwa kimataifa. Nchi zenye  uhusiano wa kidiplomasia na China zinatambua msimamo huo.

Jamhuri wa Watu wa China ni muungano wa China Bara, pamoja na maeneo mengine yenye utawala maalumu unaotokana na historia ambayo taifa hilo limepitia.

Sera ya China Moja inatekelezwa kupitia mifumo miwili ya kiutawala; msingi wake ukiwa ni jiografia, historia na matamko ya kimataifa hususani ya Umoja wa Mataifa (UN).

HongKong, Taiwan na Macao ni miongoni mwa maeneo ambayo ni sehemu ya PRC.

Kwa lugha nyepesi na kwa mujibu wa sera ya China Moja, Mtanzania akisafiri kwenda HongKong au Taiwan ama Macao, hana budi kujua kwamba huko ni nchi ya Jamhuri ya Watu wa China.

Kwa maneno mengine ni kwamba, msafiri huyo akiulizwa kama amefika China, jibu lake litakuwa ndiyo kwa sababu HongKong, Taiwan na Macao ni sehemu ya PRC, yakiwa na hadhi ya kusimamia na kujiamulia mambo yao.

Sera ya "China Moja" ilitangazwa miaka ya 1970 na imetambuliwa na Umoja wa Mataifa na nchi nyingi ikiwemo Marekani. Marekani ilianzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1979.

Kwa miaka ya karibuni, Taiwan ndiyo imekuwa ikisababisha mzozo kwa kiwango cha mataifa kutunishiana misuli ya nguvu za kijeshi, huku PRC ikisimamia kwa ukamilifu sera ya China Moja.

Taiwan ni sehemu ya China, na Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), miongoni mwa majukumu yake ya kipaumbele katika enzi mpya ni kuhakikisha lengo la China kuungana linafikiwa.

Katika mkutano mkuu wa taifa wa CPC wa 18, mwaka 2012, chama hicho kilitamka kwamba Jamhuri ya Watu wa China itaendelezwa kupitia ujenzi wa ujamaa wenye sifa za Kichina.

Katika mkutano huo, Chini ya uongozi wa kamati kuu ya CPC, hatua mpya na za kibunifu zilipitishwa kuhusiana na Taiwan, katika kuelekea kwenye muungano wa kitaifa.

Katika miaka ya karibuni, Taiwan, chini ya chama cha Democratic Progressive (DPP) imeonekana kuwa na dalili za kufuata njia ya kujitenga ikichochochewa mataifa ya nje.  

Miongoni mwa mataifa hayo ni Marekani ambayo imekuwa ikikiuka sera ya China Moja, ambayo ilitia saini kuikubali lakini matamshi na vitendo vya nchi hiyo chokochoko za kutaka kuidhibiti PRC kupitia Taiwan.

Vikosi vya kijeshi vya nchi za magharibi vimekuwa vikiitumia Taiwan kuzuia Jamhuri ya Watu wa China kupata mafanikio kamili ya kuungana na kuhuhisha mchakato wa utaifa.

Kwa mikoa ya Hong Kong na Macao, jumuiya ya kimataifa haishuhudii mzozo kama ilivyo kwa Taiwan, ambapo PRC imekuwa na mivutano na nchi za magharibi, hususani Marekani kuhusiana na kisiwa hicho.

  “Taiwan ni sehemu muhimu ya ardhi ya China,” alitamka kwa uthabiti, Rais Xi Jingping katika maadhimisho ya miaka 75 ya siku ya taifa, 2024,  huku akitoa wito wa kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kiutamaduni katika Mlango-Bahari wa Taiwan na kupinga harakati zozote za kisiwa hicho kujitenga.

China ni Moja, Taiwan ni sehemu ya China, ni ukweli usiopingika unaoungwa mkono na jiografia, historia na sheria za kitaifa na kimataifa; yoyote mwenye kujaribu kupotosha ukweli huo, atashindwa.  

TAIWAN MKOA WA 20

Simulizi zinaeleza Taiwan ni sehemu ya China, kwa sababu katika zama za kale eneo hilo lilikuwa limeungana na China Bara lakini kukatokea mabadiliko ambapo ardhi ilisogea na kuzitenganisha.

Eneo la nchi kavu lilokuwa limeunganisha pande mbili hizo, lilizama na kuwa mlango wa bahari, Taiwan ikawa kisiwa.

Utafiti mbalimbali ulifanyika ukihusisha tukio hilo na katika fukukuafukua vitu kama vyombo vilivyotengenezwa kwa mawe, kauri nyeusi na kauri za rangi mbalimbali vilipatikana.

Matokeo ya utafiti yalionyesha nakshi katika vyombo hivyo ni sawa na vile vilivyopo katika China Bara, hivyo kuchukuliwa kuwa ni uhibitisho wa watu wenye utamaduni unaofanana.

Kwa kadri miaka ilivyokuwa ikisonga mbele, tawala za kijadi za China Bara zilituma watu kwenda Taiwan na baadaye  wakazi wa pwani ya China Bara, hasa wa Quanzhou na Zhangzhou mkoani Fujiani, walikimbilia au kuhamia Penghu na Taiwan kwa ajili ya kukwepa vurugu za vita.

Mwaka 1335, utawala wa kifalme wa Yuan ulianzisha rasmi idara ya doria na uchunguzi Penghu, kwa ajili ya kusimamia mambo ya raia wa Penghu na Taiwan, na huo ukawa mwanzo wa China kuanzisha mamlaka maalumu ya utawala katika Taiwan.

Hatua kwa hatua mawasiliano kati ya watu wa China Bara na Taiwan yakaendelea siku hadi siku. Mwaka 1628, Fujiani ilipokumbwa na maafa ya ukame, wakazi wa China Bara walienda Taiwan kusaidia, wakijikita katika kilimo.

Tangu hapo Taiwan ikaingia katika kipindi cha uendelezaji mkubwa wa rasilimali na ilipofika mwaka 1684, mkoa wa Taiwan ulianzishwa chini ya mamlaka ya Fujian, na mwaka 1885 hadhi ya Taiwan iliboreshwa kuwa mkoa wa 20 wa China.

UVAMIZI WA JAPAN

Baada ya kuwa koloni la Uholanzi kwa muda mfupi, Taiwan ikawa chini ya ukoo wa Qing wa China, kabla ya kuwa chini ya Japan baada ya taifa hilo kushinda vita vya kwanza dhidi ya China.

Japan ilifanya vita dhidi ya China na kuendelea kuteka visiwa vya Taiwan na Penghu kuanzia mwaka 1931 hadi 1945. Tarehe 9 Desemba 1941, serikali ya China ilitangaza vita dhidi ya Japan na kuapa kuikomboa Taiwan, Penghu na Visiwa vya China Kaskazini vilivyotekwa nyara na Japan.

Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Japan ilijisalimisha na kuacha udhibiti wa maeneo ambayo ilikuwa imeyachukua kutoka China, na ndipo Taiwan ikatambuliwa kuwa inatawaliwa na Jamhuri ya China (ROC), ambayo ilianza kutawala kwa idhini ya washirika wake Marekani na Uingereza.

Lakini katika miaka michache iliyofuata kulizuka vita vya wenyewe kwa wenyewe China na wapiganaji walioongozwa na Chiang Kai-shek walishindwa vibaya mno na Jeshi la Kikomunisti chini ya uongozi wa Mao Zhedong.

Kutokana na kushindwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, Chiang ambaye alikuwa akiongoza chama cha Kuomintang (KMT) na wafuasi wake wanaokadiriwa kufikia milioni 1.5 walikimbilia Taiwan mwaka 1949.

Julai 26, 1945 Marekani na Uingereza walitia saini kutambua China ni moja, katika tamko maarufu la Potsdam ambalo baadaye lilitambuliwa pia na  Shirikisho la Nchi za Kisovieti.

Mwaka huo huo, Japan ilitia saini makubaliano ya kujisalimisha na kuahidi kutimiza kwa uaminifu tamko la Potsdam.

Oktoba 1, 1949, Jamhuri ya Watu wa China (PRC) ilianzishwa na kuwa mrithi wa Jamhuri ya China (ROC) iliongoza China kuanzia mwaka 1912 hadi 1949.

AZIMIO LA UN

Azimio namba 2758 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, linalojulikana kwa kichwa cha habari kisemacho “Kurejeshwa kwa Haki Halali za Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa,  Oktoba 25, 1971”, linatambua Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kama "mwakilishi pekee halali wa China kwenye Umoja wa Mataifa".

Azimio hilo ni hati inayojumuisha kanuni ya sera ya China Moja ambayo mamlaka yake hayaachi shaka na imetambulika miongoni mwa mataifa duniani kote.  

Kwa UN kupitisha azimio hilo, maana yake Taiwan ni sehemu ya PRC na haina uhalali wala haki ya kujiunga na Umoja wa Mataifa, au shirika la kimataifa lolote ambalo uanachama wake ni mataifa huru.

Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza baadhi ya mataifa ya magharibi, kinara akiwa ni Marekani yamekuwa yakipotosha Azimio 2758 kukidhi masilahi binafsi.

Yanajaribu kubadilisha uamuzi wa sheria ya kimataifa unaotambua China Moja ambayoTaiwan ni sehemu yake, na matokeo ni chokochoko zinazorudisha nyuma jitihada za China Bara kufikia azima ya kuungana.

Nchi hizo zimekuwa zikitumia suala la Taiwan kutaka kuidhibiti China na wakati wote msimamo wa PRC ni kwamba lazima Azimio la Umoja wa Mataifa linalotambua China Moja, liheshimiwe.

Kutumia Taiwan kama silaha ya kuvuruga umoja wa watu wa China, ni kitendo cha kuvunja sheria za kimataifa na ahadi za kisiasa, kunakofanywa na nchi hizo.

Mara zote serikali ya China imelaani na kuonyesha upinzani mkali dhidi ya Marekani na washirika wake wanaoharibu mamlaka ya China na kudharau kanuni za msingi za sheria za uhusiano wa kidiplomasia wa kimataifa.

Hadi sasa, nchi 183 ikiwemo Marekani wameanzisha uhusiano wa kidiplomasia na PRC kwa misingi ya kanuni ya China Moja, kwa nchi kulazimisha kutambua Taiwan kama taifa huru ni uchokozi na kuyumba kimsimamo.

Taarifa ya pamoja ya China na Marekani kuhusu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia iliyochapishwa, Desemba 1978, inasema: serikali ya Marekani inakubali msimamo wa Wachina kwamba kuna China moja na Taiwan ni sehemu ya China.

Pia inasema: Marekani inatambua Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kama serikali pekee ya kisheria ya China. Katika muktadha huo, Wamarekani watashirikiana kiutamaduni, kibiashara, na mahusiano mengine yasiyo rasmi kimataifa na Taiwan.

CPC UTI WA MGONGO

Mara baada ya kuanzishwa kwake mwaka 1921, Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) kiliweka lengo la kuikomboa Taiwan kutoka kwa utawala wa kikoloni.

Baada ya kuanzishwa kwa PRC mwaka 1949, China chini ya  uongozi wa Mao Zedong, ilipendekeza suala la Taiwan lishughulikiwe kwa  msingi wa amani. Chama hicho kilifanya mawasiliano na mamlaka ya Taiwan katika kutafuta suluhisho la suala la mkoa huo.

Katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa CPC wa 11, mwaka 1978, chini ya uongozi wa Kiongozi Deng Xiaoping, ulifafanuliwa msingi wa mwongozo wa kuungana kwa amani kwa maslahi muhimu ya China.

Ni katika mkutano huo, CPC ilianzisha dhana ya Nchi Moja, Mifumo Miwili na kuitumia katika kusuluhisha hali ilivyokuwa HongKong na Macao.

CPC kilichukua hatua za kupunguza kutunushiana msuli wa kijeshi katika Mlango-Bahari Taiwan, kurejesha mawasiliano, na kufungua milango kwa watu kutembeleana.

Katika mkutano mkuu wa CPC wa taifa wa 13, mwaka 1989, chini ya uongozi wa Rais Jiang Zemin, chama hicho kilitoa mapendekezo kwa ajili ya China kuungana kwa amani.

Chama Kikomunisti cha China, kilichukua hatua madhubuti dhidi ya harakati zilizokuwa zikifanywa na Lee Teng-Hui aliyekuwa kiongozi wa Taiwan tangu mwaka 1988 hadi 2000.

Katika mkutano mkuu wa 16 wa kitaifa wa CPC mwaka   2002, Chini ya Rais Hu Jintao, wajumbe walionyesha umuhimu wa maendeleo ya amani na uhusiano mtambuka na Taiwan.

CPC ilifanya kazi ya kuhakikisha mabadiliko yanafanyika kwa amani kwa kukuza mashauriano ya kitaasisi na mazungumzo ambayo yalizaa matunda chanya.

Baada ya mkutano mkuu wa 18 wa kitaifa wa CPC mwaka 2012, chini ya uongozi wa Xi Jinping, CPC ilitengeneza sera ya jumla ya kutatua suala la Taiwan kulingana na nyakati za sasa.

Katika mkutano wake wa kitaifa wa 19, Oktoba 2017, CPC ilithibitisha sera ya msingi ya kudumisha Nchi Moja, Mifumo Miwili na kukuza muungano wa kitaifa.

Azimio la kutoruhusu mtu yeyote, shirika lolote, chama cha siasa chochote, wakati wowote au kwa namna yoyote, kutenganisha sehemu yoyote ya eneo la China kutoka Jamhuri ya Watu wa China.

CPC na serikali ya China zimelinda amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan na maslahi ya kimsingi ya taifa la China kwa kuchukua hatua halali zenye ufanisi dhidi ya nguvu za kujitenga.

Chini ya uongozi wa CPC, maendeleo makubwa yamepatikana katika uhusiano ambao unaweza kuelezewa kuwa ni wa njia panda katika miongo saba iliyopita, kwa mafarakano kati ya pande mbili kumalizika.

Katika miaka mitatu iliyopita, CPC imekuwa uti wa mgongo wa taifa la China, kwa kutumia uongozi imara katika kufanikisha ufufuaji wa taifana kuunganishwa tena.

Hata hivyo, juhudi thabiti za CPC, kuhusu suala la Taiwan, ili kufikia muungano kamili kunategemea kuzingatiwa kwa sera ya China Moja, ambapo si mtu wala taifa au nguvu yoyote ile itapata upenyo   kutenganisha Taiwan na PRC.

Ni muhimu, CPC kujitahidi kustawisha maisha ya Wachina wote

ikiwa ni pamoja na wale wa Taiwan, na kutambua matarajio

ya watu ya kuwa na maisha bora.

CPC inasema kwamba ni muhimu kudumisha umoja na mshikamano kwa ujasiri na ujuzi wa kupigana dhidi ya nguvu yoyote inayojaribu kudhoofisha mamlaka ya Uchina.

Hata hivyo, kuongezeka kwa watu kutembeleana, ushirikiano mpana na  

mwingiliano katika nyanja mtambuka kumeleta manufaa yanayoonekana kwa watu wote wa Mlango wa Bahari, hususani wa Taiwan.

MUUNGANO KAMILI NI MUHIMU

Muungano kamili ni muhimu kwa uhuhishaji wa kitaifa

katika historia ya miaka 5,000 ya China. Katika enzi ya kisasa kutoka

katikati ya karne ya 19, kutokana na uchokozi wa Magharibi na

utawala wa kimwinyi, China ilipitia katika kipindi cha

kuteseka.

Nchi ilivumilia unyonge mkubwa, watu waliteswa

kwa maumivu makubwa, na ustaarabu wa Kichina ulitumbukia ndani

gizani.

Ukaaji wa kimabavu wa miaka 50 wa Japan katikaTaiwan ni udhihirisho wa hali hiyo, kumesababisha kuwepo kwa ‘jeraha’ la kutenganishwa lililoachwa na historia ambayo taifa la China limepitia.

Wachina kwa umoja wao wanapaswa kufanya kazi ili kufikia

kuungana na kuponya jeraha hilo kupitia uhuhishaji wa kitaifa ambao umekuwa ndoto kuu ya Watu wa China na taifa la China.

Hakuna njia nyingine itakayoweza kuzuia Taiwan kutovamiwa na kukaliwa tena na mataifa ya kigeni, isipokuwa kuungana na China Bara ili kuzima majaribio ya vikosi vya nje kuidhibiti taifa hilo.

Pengine ni wakati muafaka wa kurejea na kuitekeleza kwa dhati kauli ya Dk. Sun Yat-sen, mwanzilishi wa mapinduzi ya China kwamba “kuungana ni tumaini la raia wote wa China”.

Kwamba Wachina waunganishe nguvu, wajenge nyumba yao kwa umoja, walinde masilahi na ustawi kwa mustakabali mwema wa Jamhuri ya Watu wa China.

Rais Xi Jingping amesema kutafuta suluhu ya suala la Taiwan kuwezesha kuungana tena ni jukumu la kihistoria lenye dhamira isiyotikisika ya Chama cha Kikomunisti cha China.

“Sisi sote, wazalendo wa pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, lazima tuungane na kusonga mbele kwa umoja,” alisema kiongozi huyo katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa CPC, mwaka 1921.

Alionya kwamba, yoyote atakayethubutu kutumia nguvu kuikandamiza au kuidhibiti China, atapambana na ukuta imara wa chuma uliojengwa na Wachina zaidi ya bilioni 1.4.


Suggset To Friend:   
Print