Mwanzo > Habari kuhusu China
Rais Kikwete atuma rambirambi China
2014-03-06 15:25

RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa China, Xi Jinping, kutokana na vifo vya watu 28 vilivyosababishwa na shambulio la kigaidi hivi karibuni na kujeruhi wengine zaidi ya 130.

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilisema Rais Kikwete alimweleza Rais Xi kuwa taarifa za tukio hilo na vifo zimemsikitisha, kumhuzunisha na analaani tukio hilo.

Kikwete alisema Tanzania iko pamoja na nchi yake katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kusisitiza kuwa ipo haja ya wahusika wa tukio hilo, kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Shambulio hilo la kigaidi, lilifanyika katika eneo la wazi lililokuwa na mkusanyiko wa watu na kwenye kituo cha kukatia tiketi za treni kilichoko Kunming, katika mji mkuu wa jimbo la Yunnan, Kusini Magharibi ya China.

Suggset To Friend:   
Print