1991 Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Beijing, akisomea siasa za kimataifa, shahada ya kwanza na shahada ya uzamili.
1991-2013 Alifanya kazi katika Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya China (CIIS), Idara ya Mipango ya Sera, Idara ya Masuala ya Afrika na Idara ya Habari ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa China (MFA), alipangiwa kufanya kazi katika Ubalozi wa China nchini Kanada (Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi III), Ubalozi wa China katika nchi ya Israel (Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi II) na Ubalozi wa China katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri (Mshauri)
2014-2015 Naibu Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Utafiti ya Idara ya Kimataifa, Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China
2015-2019 Naibu Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Masuala ya Usalama wa Nje, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa China (MFA)
2019-2021 Mshauri wa Waziri, Waziri wa China nchini Kanada
2021- Balozi, Ubalozi wa China nchini Tanzania.