Mei 28, Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian alitembelea Kambi ya Wapiganaji wa Uhuru wa Harakati za Ukombozi wa Afrika, na ofisi ya tawi la Wilaya Kongwa, Mkoa Dodoma la Chama cha Mapinduzi (CCM). Alisindikizwa na Balozi Msaidizi Wang Yong na Mshauri Xu Sujiang. Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya Kongwa Musa Abdhi, Spika wa zamani wa Bunge la Kitaifa Job Ndugai, Mkuu wa Wilaya Kongwa Simon Mayeka, na Mwenyekiti wa Baraza la Wilaya Kongwa White Zuberi na viongozi vingine kutoka CCM na serikali walimuelekeza ujumbe huo katika ziara yake yote.
Pande zote mbili walikumbuka michango ya China katika ukombozi wa Tanzania na Afrika Kusini, wakasisitiza umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza historia hii, kuimarisha ushirikiano wa vyama vya kisiasa na maeneo, na kuimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Tanzania, na China na Afrika.
Kambi hiyo ilianzishwa mwaka 1964, Rais wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma, na Rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Machel wamefunzwa hapa.