Balozi Chen Mingjian na Wafanyakazi wa Ubalozi wa China Washiriki Marathon ya Siku ya Afrika 2025
2025-05-27 03:44
Mei 25, Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian na wafanyikazi wa Ubalozi wa China walishiriki katika Marathon ya Siku ya Afrika 2025, iliyoendeshwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, pamoja na Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika nchini Tanzania.
Mandhari ya Siku ya Afrika 2025, iliyothibitishwa na Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Afrika, ilikuwa "Haki kwa Waafrika na Watu wa Asili ya Kiafrika kupitia Fidia". Mhe. Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wabalozi wa Comoros, Indonesia, Kenya, Burundi nchini Tanzania na wanadiplomasia wa nchi nyingine, na washindani wa wenyeji walishiriki katika marathon hii.