Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Salamu za Mwaka Mpya 2025 za MHE. Balozi Chen Mingjian
2025-01-03 19:25

Kadri mwaka mpya unavyoanza, na sisi pia tuanze upya. Tunapoingia mwaka mpya wa 2025, kwa niaba ya Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa jina langu mwenyewe, napenda kutoa salamu za dhati na heri ya mwaka mpya kwa marafiki wote wanaoendelea kuimarisha urafiki kati ya China na Tanzania, wasomaji wenzangu wa salaam hizi, pamoja na raia wote wa Kichina, taasisi za Kichina, na wanafunzi wa Kichina walioko Tanzania!

Mwaka 2024, China ilitekeleza mpango wa maendeleo uliowekwa katika Kikao cha Tatu cha Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na kupiga hatua kubwa katika kuimarisha mageuzi kwa kina. Tukisherehekea miaka 75 tangu kuanzishwa kwa China Mpya, China iliendeleza azma yake kuu ya maendeleo ya Kitaifa na kuendelea kuifanya China kuwa kisasa kwa nguvu na dhamira.

Katika mwaka uliopita, diplomasia ya China imeendana na mwenendo wa nyakati. Sura mpya ya ajabu imeandikwa katika diplomasia ya viongozi wa kitaifa, ambayo imeelekeza mwenendo wa nyakati kuelekea amani, maendeleo, na ushirikiano wa kushinda pamoja.

Mafanikio mapya yamepatikana katika kujenga jamii yenye mustakabali wa pamoja kwa wanadamu wote.

Katika mwaka 2024, China na Tanzania zilisherehekea miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchị zetu. Ziara za mara kwa mara za viongozi wa ngazi ya juu na ushirikiano wa karibu zaidi wa vitendo zilianzisha mfululizo wa matukio ya kusherehekea miaka 60 ya uratiki wetu. Matukio haya yalijumuisha: mapokezi ya kusherehekea Miaka 60 ya Uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania, Mazungumzo ya Vijana wa China na Tanzania, Kongamano la Maendeleo ya Pamoja kati ya China na Tanzania, na Sherehe za Kufunga Mwaka wa Utalii na Utamaduni wa China na Tanzania 2024.

Pia meli kubwa yenye hospitali inayotoa huduma za afya duniani ilifika Tanzania mwaka 2024 ikiwa ni mara ya tatu kuwasili nchini. China ieendela kuwa mshirika mkubwa wa chanzo za uwekezaji Tanzania na Tanzania nayo imekuwa nayo imekuwa nchi mgeni wa Maonyesho ya kimataifa ya uingizaji na usafrikishaji bidhaa ya ClIE kwa mara nyingine tena.

Mazao ya kilimo yenye ubora wa juu kutoka Tanzania kama vile korosho, parachichi, asali yamekuwa yakiingizwa China. Mlolongo wa miradi mbalimbali ikiwemo ya daraja la Magufuli, SGR na Bwawa la Umeme la Julius Nyerere ilitekelezwa vizuri.

Mwaka 2024 pia ulishuhudia Kilele cha FOCAC kilichofanyika Beijing, ambapo China na Afrika zilishirikiana kuendeleza kisasa katika nyanja sita na hatua kumi za ushirikiano. Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping, alikutana na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliyefika nchini China kwa ajili ya kilele hicho. Viongozi wa China, Tanzania, na Zambia walishuhudia pamoja kutiwa saini kwa Hati ya Makubaliano ya Mradi wa Kutufua Reli ya TAZARA.

Mwaka 2025 ni mwaka muhimu wa kutekeleza matokeo ya Kilele cha FOCAC na pia tutashuhudia maadhimisho ya Miaka 50 ya kukamilika kwa reli ya TAZARA. Bila kujali mabadiliko ya mazingira ya dunia, China iliyostawi zaidi itaendelea kutoa msukumo kwa ushirikiano wa China na Tanzania, huku uhusiano thabiti zaidi wa China na Tanzania ukileta fursa zaidi za maendeleo ya pamoja kwa watu wetu katika nchi hizi mbili.

Tuungane mkono na kushirikiana katika kuendeleza na kuimarisha urafiki wetu wa asili katika ukurasa mpya kwa kuzungumzia changamoto na uzitatua kuelekea maendeleo na

kuchangia kuzijenga China, Tanzania na China Afrika kuwa karibu zaidi.

Mwaka wa Nyoka wa Kichina unakaribia. Katika mila za Kichina, mwaka wa nyoka unajulikana kwa utulivu. Tunatumai kuwa mahusiano ya China na Tanzania yatazidi kuimarika! Tunawatakie heri katika mwaka huu mpya marafiki zetu wote, familia zenu.

HERI YA MWAKA MPYA.

Suggset To Friend:   
Print