Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Balozi Chen Mingjian: Maendeleo ya China kuleta mustakabali mzuri siku zijazo
2022-10-31 14:59

Tarehe 29 Oktoba 2022, makala ya Balozi Chen Mingjian yenye kichwa cha habari “Maendeleo ya China kuleta mustakabali mzuri siku zijazo” ilichapishwa na gazeti la Uhuru.  Hapa kuna nakala kamili:

Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), uliofanyika Beijing kuanzia tarehe 16 hadi 22 Oktoba 2022 umefikia tamati kwa mafanikio. Ukiwa mkutano wenye umuhimu mkubwa, unafanyika wakati muhimu China inapoanza safari mpya ya kujijenga kuwa nchi ya maendeleo ya kisasa ya ujamaa katika mambo yote na maendeleo kuelekea Lengo la Karne ya Pili. Uliidhinisha Ripoti iliyowasilishwa na Katibu Mkuu Xi Jinping na kupitisha Azimio la Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China. Katika Mkutano wa Kwanza wa Mjadala wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC, Kamati Kuu mpya ya CPC ilichaguliwa na Xi Jinping akachaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu. Kufanyika kwa mafanikio kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China kunahusiana na mustakabali na hatima ya ujamaa wenye sifa za Kichina na vilevile ufufuaji mkubwa wa taifa la China. Pia utakuwa na matokeo muhimu na makubwa kwa amani na maendeleo ya dunia pamoja na maendeleo ya binadamu.

1. Ni Mkutano unaojengwa kwenye mafanikio ya zamani ili kusonga mbele, ukitoa kwa kina muhtasari wa mabadiliko ya ajabu nchini China katika zama mpya za muongo uliopita.

Katika Ripoti kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, Katibu Mkuu Xi Jinping ametoa muhtasari wa mabadiliko makubwa katika nyanja 16 za muongo mmoja uliopita tangu Mkutano Mkuu wa 18, akionyesha kwa kina maendeleo na utendaji wa ujamaa yenye sifa za Kichina katika zama mpya. Muongo uliopita uliadhimisha matukio makuu matatu yenye umuhimu mkubwa na umuhimu wa kihistoria kwa ajili ya Chama na wananchi. Tuliazimisha miaka mia moja ya CPC; tulianzisha zama mpya za ujamaa wenye sifa za Kichina; na tukaondoa umaskini uliokithiri na kumaliza kujenga jamii yenye ustawi wa wastani katika mambo yote, hivyo kukamilisha Lengo la Karne ya Kwanza. Haya yalikuwa mafanikio ya kihistoria, mafanikio yaliyofanywa na CPC na watu wa China wakijitahidi kwa umoja, na mafanikio makubwa ambayo yangerekodiwa milele katika historia ya China.

Katika muongo uliopita, Pato la Taifa la China limekua kutoka yuan trilioni 54 hadi yuan trilioni 114, ambayo ni asilimia 18.5 (kutoka 11.3%) ya uchumi wa dunia.  China imechangia wastani wa 38.6% katika ukuaji wa kimataifa kila mwaka.  Takriban wakazi milioni 100 maskini wa vijijini wameondolewa katika umaskini. China imehakikisha hali kamili na ya kudumu ya utimilifu, furaha, na usalama kwa watu wake. China imeshuhudia mafanikio makubwa kwenye nyanja kama vile safari ya anga ya binadamu, uchunguzi wa Mwezi na Martian. China imejiunga na safu ya nchi za ubunifu duniani. Mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ya zama mpya ni hatua muhimu katika historia ya Chama, Jamhuri ya Watu wa China, mageuzi na ufunguzi wa maendeleo ya ujamaa, na maendeleo ya taifa la China.

2. Ni mkutano tangulizi na bunifu, unaofafanua kwa kina na kwa utaratibu vipengele muhimu na msukumo muhimu wa njia ya Kichina kuelekea maendeleo ya kisasa.

 Katibu Mkuu Xi Jinping amesema katika Ripoti kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, "Kuanzia leo na kuendelea, kazi kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China itakuwa kuwaongoza watu wa makabila yote ya China katika juhudi za pamoja kutimiza Malengo ya Karne ya Pili ya kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kisasa ya ujamaa kwa njia zote na kuendeleza ufufuaji wa taifa la China katika nyanja zote kupitia njia ya China kuekea maendeleo ya kisasa.

Maendeleo ya kisasa ni harakati ya kawaida ya nchi zote duniani, na lengo ambalo watu wa China wamekuwa wakijitahidi kwa bidii katika nyakati za kisasa.  Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, China imefanikiwa kuendeleza na kupanua njia ya China kuelekea maendeleo ya kisasa na kuwa njia isiyoweza kutenduliwa ya ufufuaji wa taifa la China. Ni ipi njia ya Kichina kuelekea maendeleo ya kisasa?  Katibu Mkuu Xi Jinping amesisitiza kuwa ni ujamaa wa kisasa unaofuatwa chini ya uongozi wa CPC. Ina vipengele ambavyo ni vya kawaida kwa michakato ya maendeleo ya kisasa ya nchi zote, lakini inasifika zaidi kwa vipengele ambavyo ni vya kipekee kwa muktadha wa Kichina.  Ni maendeleo ya kisasa ya idadi kubwa ya watu, ustawi wa pamoja kwa wote, maendeleo ya kimaadili na kitamaduni, uhusiano kati ya binadamu na asili, na maendeleo ya amani.

Njia ya Kichina kuelekea maendeleo ya kisasa inatia mizizi katika ardhi kubwa ya China.  Sambamba na uhalisia wa China, inaendelea kuweka maendeleo ya nchi na taifa kwenye msingi wa nguvu zake yenyewe, na kuwezesha China kufahamu kwa uthabiti hatima ya maendeleo yake na kwenda mbele.  Mafanikio ya utendaji wa  njia ya Kichina kuelekea maendeleo ya kisasa yanaonyesha kuwa maendeleo ya kisasa si hati miliki inayomilikiwa na nchi za Magharibi, na kila nchi inaweza kujitegemea kutafuta njia ya kisasa inayofaa kwa hali yake ya kitaifa.  Njia ya Kichina ya maendeleo ya kisasa imetengeneza aina mpya ya maendeleo ya binadamu, kupanua njia za nchi zinazoendelea kuelekea maendeleo ya kisasa, na kutoa ufumbuzi wa Kichina kwa nchi duniani kote kuchunguza mfumo bora wa kijamii.

3. Ni mkutano unaojali watu duniani kote, unaotoa mwongozo wa maendeleo ya diplomasia ya China katika zama mpya.

Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC umetunga sera kuu na kuweka mipango ya kina kwa ajili ya maendeleo ya CPC na malengo ya China katika kipindi cha miaka mitano ijayo au hata zaidi, ambao imefafanua kwa uwazi dhamira na kazi ya "kukuza amani na maendeleo ya dunia na ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa wanadamu”.  Katika Ripoti kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, Katibu Mkuu Xi Jinping anatoa wito wa dhati kwa "nchi zote kuthamini maadili ya pamoja ya binadamu ya amani, maendeleo, haki, usawa, demokrasia na uhuru;  kukuza maelewano na kuunda uhusiano wa karibu na watu wengine;  na kuunganisha nguvu ili kukabiliana na aina zote za changamoto za kimataifa." Pia anasema kwa dhati kwamba "Wachina wako tayari kufanya kazi bega kwa bega na watu kote ulimwenguni ili kuunda mustakabali mzuri zaidi wa ubinadamu", ambayo inaonyesha kikamilifu imani thabiti ya CPC katika kutafuta maendeleo kwa wanadamu.

Katika safari mpya katika zama mpya, China itasimama kidete kufuata sera huru ya mambo ya nje ya amani, kujitahidi kushikilia kanuni za msingi zinazosimamia uhusiano wa kimataifa na kulinda haki na uadilifu wa kimataifa. China itazingatia Misingi Mitano ya Kuishi Pamoja kwa Amani katika kutafuta urafiki na ushirikiano na nchi nyingine.  Imejitolea kukuza aina mpya ya mahusiano ya kimataifa, kuimarisha na kupanua ushirikiano wa kimataifa kulingana na usawa, uwazi na ushirikiano. Ikiongozwa na kanuni za unyoofu, matokeo ya kweli, mshikamano na imani nzuri, na kwa kujitolea kwa maslahi makubwa zaidi na ya pamoja, China itajitahidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi nyingine zinazoendelea na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea. China itajitolea kwenye sera yake ya msingi ya kitaifa ya kufungua kwa ulimwengu wa nje na kufuata mkakati wa kunufaishana wa kufungua. Itajitahidi kuunda fursa mpya kwa ulimwengu na maendeleo yake yenyewe, na kuchangia sehemu yake katika ujenzi wa uchumi wazi wa kimataifa ambao unatoa faida kubwa kwa watu wote. China itashiriki kikamilifu katika mageuzi na maendeleo ya mfumo wa utawala wa kimataifa na kudumisha umoja wa kweli wa pande nyingi. China imeweka mbele Mpango wa Maendeleo ya Dunia na Mpango wa Usalama wa Kimataifa, na iko tayari kufanya kazi na jumuiya ya kimataifa ili kuweka mipango hii miwili katika vitendo.

China na Tanzania ni marafiki na washirika wakubwa, huku CPC na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni marafiki wa karibu. MH. Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan amempongeza Katibu Mkuu Xi Jinping kwa kufanikiwa kuchaguliwa tena kwa wakati, huku Katibu Mkuu Daniel Godfrey Chongolo akimpongeza Waziri wa Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CCM, Liu Jianchao, kwa kuhitimisha kwa mafanikio Mkutano Mkuu wa 20, wakienzi tena urafiki wa kina kati ya vyama viwili na nchi hizo mbili. China inapenda kutumia Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC kama fursa ya kuimarisha mabadilishano na Tanzania kuhusu utawala bora, kubadilishana uzoefu katika kuchunguza njia ya maendeleo ya kisasa, na kuiunga mkono kwa dhati Tanzania katika kuchukua njia ya maendeleo inayoendana na hali yake ya kitaifa. China iko tayari kufanya kazi pamoja na Tanzania kutafuta manufaa zaid