Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Sherehe ya 3 ya Utoaji Tuzo ya Balozi wa China 2020 Afanyika
(2020.10.20)
2020-10-22 21:12

Oktoba 20, Sherehe ya 3 ya Utoaji Tuzo ya Balozi wa China 2020 ilifanyika katika Ubalozi wa China nchini Tanzania. Mhe. Wang Ke, Balozi wa China, DkT. Leonard Akwilapo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania, DkT Liuyan, Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wawakilishi wa wanifunzi na walimu waliopewa tuzo kutoka Taasisi za Confucius nchini Tanzania, na waandishi wa habari walihudhuria hafla hiyo.

Balozi Wang aliwapongeza waliopewa tuzo, na akasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, mabadilishano ya kielimu kati ya China na Tanzania yameendelea kuongezeka, idadi ya wanaojifunza Kichina nchini Tanzania imekuwa ikiongezeka, kiwango cha ufundishaji Kichina nchini Tanzania kimeendelea kuboreshwa. Tangu mwisho wa Juni mwaka huu, shule na vyuo vikuu nchini Tanzania zimefungua tena, waalimu na wanafunzi wa Taasisi za Confucius wameshinda shida mbalimbali, na kufanya bidii kuzoea kazi na kusoma chini ya janga COVID19, na kupata matokeo mazuri. Hasa, John Magongew kutoka Shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha alishika nafasi ya 30 bora ulimwenguni na 6 bora barani Afrika katika Mashindano ya Kichina kwa Wanafunzi wa shule za sekondari duniani yaliyofanyika hivi karibuni, ambalo ni ya kufurahisha. Ili kuwahimiza zaidi wanafunzi wa Tanzania na walimu wa Kichina wa ndani, ubalozi uliongezea idadi ya tuzo na kiwango cha tuzo mwaka huu, na kuwazawadia walimu wa hapa kwa mara ya kwanza. Inatarajiwa kuwa kazi ya Taasisi za Confucius nchini Tanzania itapate maendeleo mema zaidi, na wanafunzi wanaopenda Kichina watasoma kwa bidii zaidi na kupata fursa za kusoma China, na kuchangia kukuza ushirikiano na urafiki kati ya nchi hizi mbili, Balozi Wang alisema.

Kwa niaba ya Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu ambaye anashughulikia mambo ya uchaguzi, aliishukuru serikali ya China kwa juhudi zake zote za kuendeleza ushirikiano wa elimu kati ya China na Tanzania. Alisema kuwa Taasisi za Confucius nchini Tanzania zimekuza idadi kubwa ya vipaji vya lugha ya Kichina, na inafurahi kuona kwamba vyuo vikuu vya China pia vimefungua masomo ya Kiswahili, ambalo limekuwa na jukumu muhimu katika kukuza mawasiliano na uelewano kati ya watu wa China na Tanzania. Alitumia kuwa pande hizo mbili zitaendelea kukuza ushirikiano wa kirafiki kupitia ubadilishanaji wa lugha na anatumahi kuwa waalimu na wanafunzi waliopewa tuzo watafikia matarajio yao na kukuza kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji Kichina katika shule na vyuo vikuu vya Tanzania, wakijitahidi kuwa wajumbe wa urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mashana Glory na Imani Haji wanaowakilishi wanafunzi na walimu kupewa tuzo walishiriki hadithi zao kuhusu kujifunza Kichina kwenye hafla ya utoaji tuzo. Walisema kujifunza Kichina ni furaha na ya maana, na wanajivunia kujifunza lugha hii na kuelewa utamaduni wa China.

Mwaka huu, wanafunzi 115 na waalimu 7 wa Kichina kutoka Taasisi za Confucius katika UDSM na UDOM, Darasa la Confucius katika Chuo Kikuu cha Kiislamu na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, na Programu ya Kufundisha Lugha ya Kichina katika sekta ya elimu ya msingi nchini Tanzania walitunukiwa. TBC, Daily News, Guardian zimeripoti tukio hilo.

Suggset To Friend:   
Print