Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mlipuko wa COVID-19, 13 Februari
2020-02-14 01:07

(13 Februari)

Mnamo tarehe 12 Februari, China bara, kesi 59,804 zilisibitishwa kuripotiwa, kati yao 5,911 walipona na kuruhusiwa kutoka hospitalini, 1,367 walikufa, na 52,526 bado wanaendelea kupata matibabu. Hadi tarehe 12 kulikuwa na kesi 13,435 walioshukiwa zinazosubiri majibu ya vipimo China bara. Huko Hong Kong, Macao na Taiwan, kesi zilizothibitishwa kuripotiwa ni 50, 10 na 18 mtawalia mnamo tarehe 12 Februari.

Mnamo tarehe 12 Februari, kesi zilizothibitishwa katika jimbo la Hubei ziliongezeka kufikia 14,840, juu sana kuliko ile ya siku iliyopita, 1,638. Sababu ni kuingizwa kwa kesi zilizopimwa kliniki. Kesi zilizopimwa ni za kipekee kwa Hubei kitakwimu. Kulingana na toleo la hivi karibuni la utambuzi na mpango wa matibabu uliotolewa na Tume ya Kitaifa ya Afya ya China, kesi zozote zinazoshukiwa zilizo na matokeo ya skirini inayohusiana na nimonia (CT) huhesabiwa kama kesi za vipimo vya kliniki. Tume ya afya ya jimbo la Hubei imesema marekebisho ya viashiria vya vipimo yamefanywa ili kuwapa wale ambao wamegunduliwa kliniki matibabu ya kiwango cha kawaida kwa kesi zilizothibitishwa ili kuboresha zaidi kiwango cha mafanikio ya matibabu.

Februari 12, Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC iliketi kwa mara ya tatu kujadili hali ya kuzuia na kudhibiti COVID-19. Ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping, mkutano huo ulionyesha umuhimu wa kulitatua fumbo la kudhibiti janga kwa kuinua viwango vya kulaza wagonjwa hospitali na viwango vya tiba na kupunguza maambukizi na viwango vya vifo. Ilitoa wito wa juhudi za kuboresha matibabu kwa wagonjwa, haswa walio katika hali mbaya, kwa kutumia rasilimali bora zaidi za kitabibu na kiteknolojia, kufanya mapitio ya wakati mwafaka wa suluhiho la utambuzi na matibabu na kuongeza maendeleo ya dawa na chanjo.

Kwa idhini ya Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Jeshi la China, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) linatuma wafanyakazi wa matibabu zaidi ya 2,600 kusaidia vita dhidi ya mlipuko wa COVID-19 huko Wuhan. Ujumbe wa matibabu wa PLA unashughulikia hospitali mbili katika mji huo na utafanya kazi chini ya Hospitali ya Huoshenshan, ambayo ni hospitali ya kwanza ya muda iliyoanzishwa mapema Februari wakati wa janga hilo. Kufikia tarehe 13 Februari, Jeshi la Ukombozi la Watu a China (PLA) limepeleka vikundi vitatu vya wafanyikazi zaidi ya 4,000 wa matibabu Wuhan tangu kuzuka kwa janga hilo.

Suggset To Friend:   
Print