Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya vya Corona, 10 Februari
2020-02-10 17:09

(10 Februari)

Mnamo tarehe 9 Februari, ndani ya China bara, kesi 40,171 zilisibitishwa kuripotiwa, kati yao 3,281 walipona na kuruhusiwa hospitalini, 908 walikufa, na 35,982 bado walikuwa wakiendelea na matibabu. Mnamo tarehe 9 Februari kulikuwa na kesi 23,589 za walioshukiwa zinazosubiri majibu ya vipimo. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa kati ya tarehe 4 na 9 Februari, idadi ya kesi mpya zilizothibitishwa nje ya jimbo la Hubei ziliendelea kupungua kwa siku sita mfululizo. Kufikia tarehe 9 Februari, hakuna kesi yoyote iliyothibitishwa au ya kutuhumiwa kuambukizwa virusi vipya vya corona ilikuwa imeripotiwa miongoni mwa raia wa Tanzania nchini China na hakuna kesi kama hiyo iliyoripotiwa nchini Tanzania.

Kufikia tarehe 5 Februari, viongozi wa nchi 61, akiwemo Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, na wakuu wa asasi nane za kimataifa waliandika barua kwa Rais Xi Jinping, Waziri Mkuu Li Keqiang na wanachama wengine wa uongozi wa China kuelezea mshikamano na uungwaji mkono. Walizungumza kwa uwazi kuunga mkono China na walipongeza juhudi za kudhibiti mlipuko huo . Timu ya awali ya wataalam wa kimataifa inayoongozwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) imeondoka kwenda Beijing kusaidia China kupigana na mlipuko huo.

Serikali ya China imefanya kazi kubwa kuhakikisha usalama na afya ya raia wa kigeni. Jimbo la Hubei limeanzisha simu za moja kwa moja za masaa 24 kwa raia wa kigeni na wanafunzi huko, na imekua ikitoa taarifa mpya katika lugha nyingi kuhusu kuzuka na njia za kuzuia maambukizo kwenye tovuti yake ya serikali. Majimbo na manispaa ikiwemo na Beijing, Shanghai, Tianjin, Guangdong, Jiangsu, Xinjiang wameongeza juhudi za kutoa habari na huduma kwa wageni, ambao mahitaji yao katika suala la maisha ya kila siku, kujilinda na matibabu yanapatikana. Raia wa kigeni wako salama nchini China.

Kulingana na tathmini ya kitaalam ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros, njia salama kabisa kwa raia wa kigeni huko Wuhan ni kutulia na kuhakikisha usalama wa kujikinga. Ameonya dhidi ya harakati za haraka haraka kwani itaongeza kutokuwa na uhakika. Kesi zilizothibitishwa zimepatikana kati ya baadhi ya watu wanaotokea nje, ambazo zinaongeza hatari ya kuenea zaidi.

Kuna uvumi kadhaa unaovuma kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania zinazohusiana na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya vya Corona. Kama vile Dk Tedros alivyoiweka sawa, virusi vinaogopeka, lakini kinachotisha zaidi ni uvumi na hofu kubwa . Serikali ya China inatoa habari zinazohusiana na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya vya Corona kwa njia ya uwazi. Tafadhali USIAMINI uvumi huo na ujulishwe na vyanzo rasmi na vya kuaminika, ikiwemo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ubalozi wa China nchini Tanzania, nk.

Virus hivi siyo vya kawaida, na hali kadhalika hatua tulizo chukua kubaliana na mlipuko huo, kuna maneno manne muhimu: tulia, pumzika, jiamini na uwe mvumilivu.

Suggset To Friend:   
Print