Mwanzo > Habari Mpya za ubalozi wa China
Udhalimu wa kibiashara unawaweka uchumi wa kimataifa hatarini, lakini hauwezi kurudisha nyuma ukuaji imara wa China
2019-06-22 01:35

Hivi karibuni, Mhe .Bi. Wang Ke, Balozi wa China alikubali mahojiano maalum na Mwananchi juu ya msuguano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani.

 

Mwandishi: Msuguano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani umekuwa tukio lililopewa umakini zaidi duniani. Watu wanashangaa kwa nini mgogoro huo hauwezi kuepukika, licha ya ukweli kwamba mazungumzo ya uchumi na biashara ya nchi mbili yalizinduliwa mwezi Februari 2018 na yamepitia hatua 11? Nani wakulaumiwa kwa hali ya sasa?

Balozi Wang:

Tokea ulipoanza kazi mwaka 2017, utawala mpya wa Marekani umetishia kuongeza ushuru na hatua zingine na kuchochea mara kwa mara msuguano wa uchumi na biashara na washirika wake wakuu wa biashara. Kwa kukabiliana na msuguano wa kiuchumi na kibiashara wa upande mmoja ilioanzishwa na Marekani tangu Machi 2018, China ilibidi kuchukua hatua za nguvu kulinda maslahi ya taifa na watu wake. Wakati huo huo, nia ya kusuluhisha migogoro kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, China imejihusisha katika mazungumzo mengi ya uchumi na biashara na Marekani kwa jitihada za kuimarisha uhusiano wa biashara wa nchi mbili.

Mashauriano ya uchumi na biashara yametoka mbali huku pande hizo mbili zikikubaliana sehemu kubwa ya mkataba. Lakini mashauriano hayajakosa matatizo, kila moja ikiwa ni matokeo ya Marekani kuvunja makubaliano na ahadi, na kurudi nyuma. Ni dhahiri kwamba ahadi zingine zimevunjwa, sio na China bali na wale wanaoshikia bango ushuru dhidi ya China.

China inatatua tofauti kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, kwa sababu hii ni kwa maslahi si ya China na Marekani pekee bali pia jumuiya ya kimataifa. Katika hali ya vitisho vya Marekani kuongeza ushuru, China bado ilituma ujumbe wa ngazi ya juu kwa Marekani kwa ajili ya mazungumzo kama ilivyokubaliwa, ikiangazia mtizamo mpana, uaminifu wa hali ya juu na utashi.

Inasikitisha, Marekani ilifanya shinikizo la juu wakati wa mazungumzo ya awali, ilisisitiza juu ya kupigana vita ya biashara ya upande mmoja na kuingilia katika vitendo vya unyanyasaji. Kwa upande mwingine, upande wa Marekani umekuwa ukigeuka katika meza ya mazungumzo, na kuendelea kuipaka matope China kwa kutoa taarifa za kupotosha katika mazungumzo na kutofikia muafaka, ikilenga kufunika makosa yake mwenyewe. Hata hivyo, tuhuma za China kubadili mawazo yake hazina ukweli kabisa. Awali, zaidi ya hatua kumi za mazungumzo, utawala wa Marekani uliendelea kubadilisha mahitaji yake. Uzoefu wa kihistoria umethibitisha kwamba jaribio lolote la kulazimisha mpango kupitia mbinu kama vile kuchafuana, kudhoofisha na shinikizo la juu zitaharibu uhusiano wa ushirika.

Mnamo Juni 2, serikali ya China ilitoa msimamo wake (white paper) ili kuonyesha picha halisi ya ushauri wa uchumi na biashara baina ya China na Marekani kwa mtazamo wa usawa na mantiki, na msimamo wa sera ya sasa ya China juu ya mashauriano haya. Ninapendekeza marafiki wa Tanzania wanaofuatilia jambo hili wausome huu msimamo (white paper) ili kupata ufahamu kamili.

Mwandishi: Je! Msuguano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani utakuzwa? Ikiwa ndivyo, ni kwa namna gani uchumi wa China utaathirika, na China inaweza kukubaliana au kukubali ili kuepuka uharibifu?

Balozi Wang:

Kama nilivyosema hapo awali, Marekani inapaswa kubeba jukumu la pekee na lote la mvutano wa sasa. Kwa hiyo, ikiwa msuguano utaongezeka au kupungua pia itategemea maamuzi na matendo ya Marekani.

China haitaki "vita ya biashara" lakini haiogopi mtu na inaweza kupigana na mtu ikiwa ni lazima. Mnamo Mei, China ilitangaza kuwa itatoza ushuru wa ziada wa dola bilioni 60 ya mauzo ya Marekani kutoka Juni 1. Uamuzi huo ulikuja baada ya hatua ya Marekani kuongeza ushuru wa dola bilioni 200 za bidhaa za China kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25.

Huu ni ushahidi wa ulinzi wa haki dhidi ya udhalimu wa kibiashara wa Marekani na kutetea taratibu za biashara za kimataifa na kulinda haki na maslahi yake. China itachukua hatua za lazima zinazofaa ikiwa hali itaendelea kuzorota.

Akizungumza pasipo upendeleo, bila shaka hatua ya Marekani itaweka ushawishi hasi juu ya uchumi wa China. Kama baadhi ya taasisi za soko zinavyotabiri, msuguano unatarajiwa kupungua chini ya kiwango cha wastani wa ukuaji wa Pato la Taifa la China kwa asilimia 0.2 hadi 0.65. Hata hivyo, hatua ya Marekani haiwezi kubadili au kurekebisha ukuaji imara wa China kwakuwa mauzo ya nje ya China yanatawanywa na mabadiliko ya uchumi yanayoendelea taratibu na kwa hatua yakiambatana na mageuzi makubwa. China inajiamini katika kukabiliana na matatizo yaliyo mbeleni, kuzidabili hatari na kuwa fursa,na kufungua ukurasa mpya.

China kamwe haitoshindwa katika masuala ya kanuni. Tunasisitiza kuwa uhuru wa nchi na hadhi lazima viheshimiwe wakati wa mashauriano, na makubaliano yoyote yaliyofikiwa na pande zote lazima yazingatie usawa na manufaa ya kila upande. China haitoshindwa dhidi ya mahitaji yasiyo na maana ambayo yatahatarisha maslahi yake ya msingi na haki halali za maendeleo, na kamwe haitojisalimisha kufuatia vitendo vya kidhalimu na shinikizo la juu kutoka Marekani.

Mwandishi: Unatarajia nini kutokana na mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani?

Balozi Wang:

Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu tangu biashara na msuguano vilipoanza, upande wa China umekuwa mara zote ukionyesha kuzuia na kuzingatia mashauriano kwa misingi ya usawa, kuheshimiana, na imani nzuri. Napenda kusema kwamba, mlango wa fursa haufungwi lakini hautakuwa wazi daima . Tunatakiwa kutarajia mazuri zaidi na kujiandaa kwa mabaya zaidi.

Ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa China na Marekani na kila upande kunufaika kwa usawa ni njia pekee bora ya baadaye. Na kuhusu wapi mashauriano ya kiuchumi na ya kibiashara ya China na Marekani yanapoelekea, China inaangalia mbele, sio nyuma. Migogoro na mifarakano juu ya biashara na uchumi mbeleni, mwishoni mwa siku, inahitaji kutatuliwa kupitia mazungumzo na mashauriano. Kupungua kwa faida za kila upande na makubaliano ya kila upande kunufaika vinatumika kwa maslahi ya China na Marekani na kufikia matarajio ya dunia. Inatarajiwa kuwa Marekani inaweza kwenda mwelekeo sawa na China, katika mtizamo wa kuheshimiana, usawa na manufaa ya pamoja, kusimamia tofauti za uchumi na biashara, kuimarisha ushirikiano wa biashara na uchumi, na kuendeleza mahusiano ya pamoja ya China na Marekani kwa kuzingatia uratibu , ushirikiano na utulivu kwa ustawi wa mataifa hayo na dunia.

Mwandishi: Mnamo tarehe 15 Mei, Idara ya Biashara ya Marekani iliongeza Huawei kwenye orodha ya makampuni ambayo Makampuni ya Amerika hayawezi kufanya biashara bila ruhusa rasmi. Nini madhumuni halisi ya sera ya Marekani ya kupiga marufuku Kampuni kubwa ya teknolojia ya Kichina?

Balozi Wang:

Ikiwa na wasiwasi kuhusu nafasi ya Huawei katika teknolojia ya mtandao ya 5G, na maslahi binafsi ya kudumisha kile kinachojulikana kama "Amerika Kwanza", Marekani inatumia ukiukwaji wa nguvu zake na marejeo ya sheria zake za ndani kuchukua "mamlaka ya mahakama zake kimipaka kuhusu mtuhumiwa" juu ya Huawei.

Katazo juu ya Huawei lililofanywa na Marekani ikisingizia usalama wa taifa halina msingi, bila ya kutumia akili ya kawaida na isiyo na mantiki. China inayaambia makampuni ya Kichina kufuata sheria na kanuni juu ya udhibiti wa kuuza nje na kutimiza majukumu yetu ya kimataifa. China pia inazitaka makampuni ya Kichina kufuata sheria za mitaa za nchi na sera wakati wa kufanya biashara nje ya nchi. Lakini wakati huo huo, tunapinga tendo la nchi yoyote ya kulazimisha vikwazo juu ya nchi ya China kwa kutumia sheria zake za ndani, na kutumia vibaya hatua za udhibiti wa biashara nje ya nchi wakati ikiufanya "usalama wa taifa" kama kila kitu. Tunaisihi Marekani kurekebisha tendo lake baya la kutumia nguvu za serikali kudidimiza biashara za kigeni, kutafuta uhalali kinyume cha sheria, kuharibu soko na kudhoofisha ushirikiano wa kimataifa.

Ni dhahiri kwamba Marekani imekuwa ikiichafua kampuni ya Huawei ikijaribu kupata faida kutokana na ushindani usio wa haki. Lakini imeshindwa kuzalisha ushahidi wowote. Tunafurahi zaidi kuona kwamba serikali za kigeni, vyombo vya habari na watu wamesema maneno ya busara na ya haki juu ya suala la Huawei. Kulingana na maoni ya umma ya hivi karibuni ya CNN, asilimia 61 ya Wamarekani wanaamini kwamba serikali ya Marekani kupiga marufuku Huawei kumetokana na motisha za kisiasa. Baadhi ya vyombo vya habari vya Ujerumani pia vimetoa taarifa kwamba baada ya miaka ya ukaguzi, Uingereza, Ujerumani na Umoja wa Mataifa hawakuweza kupata udhaifu wowote katika bidhaa za Huawei. Hizi zimeshuhudia Huawei kutokuwa na hatia na kuweka wazi ukosefu wa uhalali wa Marekani wa kutokomeza Huawei kwa nguvu za serikali.

Mwandishi: Kama mataifa yenye uchumi mkubwa na mataifa ya biashara duniani, ni jinsi gani msuguano wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani utaathiri uchumi wa dunia na biashara, hasa uchumi wa Afrika?

Balozi Wang:

Biashara kati ya mataifa mawili yenye uchumi mkubwa duniani sio muhimu tu kwa China na Marekani lakini pia ina ushawishi kwenye uchumi mwingine wote ulimwenguni. Kitu ambacho Marekani inachofanya pia kinaweka uchumi wa kimataifa hatarini. Taasisi nyingi za kimataifa zina wasiwasi kwamba ikiwa mgogoro huu wa nchi mbili utaendelea au kuongezeka, viwanda na minyororo ya thamani duniani inaweza kupungua, uwekezaji na biashara ya nje ya mipaka inaweza kuathirika na kukua kwa uchumi wa dunia kunaweza kupungua.

Hakuna uchumi ambao ungeweza kupona ikiwa kushuka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi na biashara imetokea duniani kote, ikiwa ni pamoja na Afrika. Wataalam wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wanaonya kwamba mvutano wa biashara kati ya China na Marekani unaweza kupunguza asilimia 2.5 katika Pato la Taifa katika nchi za Afrika zenye wingi wa rasilimali na kupunguza asilimia 1.9 kwa wauzaji wa mafuta kwa mwaka wa 2021. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pia lilionya kuwa vita ya biashara peke yake inaweza kusababisha asilimia 1.5 ya kushuka kwa ukuaji wa pamoja wa Pato la Taifa la Afrika kwa mwaka 2021. Marafiki wengine wa Tanzania tayari wameelezea wasiwasi wao kuhusu "nyasi zitapata shida sana wakati tembo wanapigana juu yake".

Kitu kibaya zaidi ni kwamba vita za biashara za Marekani pekee zimeweka mfano mbaya, na kudhoofisha sana siasa za kimataifa, utaratibu wa uchumi na biashara. Kushikia bango swala la ushuru dhidi ya China kwa manufaa yake ya leo, Marekani pia itaweka vikwazo kwa nchi yoyote ambayo inadhaniwa kuwa mpinzani kwa maslahi yake katika siku zijazo. Kwa kweli, Marekani sasa inatishia kuongeza ushuru si tu kwa China lakini pia katika Umoja wa Ulaya, Japan, Mexico, na India nk.

Madhumuni ya kweli ya tabia hii ya udhalimu ni kulinda maslahi yake ya ziada ya nguvu kupitia njia zisizo za haki. Huu ni ukatili mkali juu ya matakwa mazuri ya kupata maisha mazuri kupitia kazi ngumu za watu wa nchi nyingine. Ninaamini kwamba mtu yeyote mwenye haki mwenye dhamiri hatakubaliana na hili.

Haijalishi jinsi mazingira ya nje yanavyoendelea, hatua ya ushirikiano wa China na Afrika haitosimama. China itaendelea kufanya kazi pamoja na nchi za Kiafrika ili kufikia maendeleo ya kawaida kupitia ushirikiano wa kila upande kunufaika. Ni matumaini yetu kuwa Marekani inaweza kukutana na China katikati na kuunganisha nguvu za pamoja kukuza maendeleo Afrika.

Suggset To Friend:   
Print