Taarifa Kwa Umma
Aprili 4, 2019
Kukusanya insha nyingi zaidi na kuruhusu watu zaidi wawe na nafasi ya kushiriki katika "Kumbukumbu za Urafiki wa China na Tanzania" Shindano la Uandishi wa Insha, Ubalozi wa China nchini Tanzania, baada ya kushauriana na waandaji wengine wa Shindano hilo, umeamua kuongeza tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kuwa Mei 15, 2019. Washiriki wenye uwezo wanakaribishwa kuwasilisha insha zao kabla ya tarehe ya mwisho. Tumefanya marekebisho kwa mahitaji ya insha zinazoshiriki. Mahitaji mapya ni kama ifuatavyo:
1. Mwandishi anapaswa kuwa raia wa China au wa Tanzania.
2. Insha inatakiwa kuongelea hadithi moja au kadhaa zinazohusiana na urafiki wa China na Tanzania.
3. Insha zinapaswa kuandikwa kwa Kichina, Kiswahili au Kiingereza.
4. Urefu wa insha lazima uwe chini ya au takribani maneno 2,000 ya Kichina au maneno 2,000 ya Kiswahili au Kiingereza.
5. Kila mshiriki atawasilisha kazi moja tu na picha 3 au video moja zikiambatanishwa. Ukubwa wa picha haipaswi kuzidi MB 5, na video haipaswi kuzidi dakika 2. Picha na video zinapaswa kuendana na hadithi zilizopo katika insha na kutumwa kwa kutenganishwa na insha.
6.