Mwanzo > Rolling News Report
Taarifa ya Kuongezwa kwa Muda wa Uwasilishaji wa shindano la Uandishi wa Insha "Kumbukumbu za Urafiki wa China na Tanzania"
2019-04-04 22:45

Taarifa Kwa Umma

 

Aprili 4, 2019

 

Kukusanya insha nyingi zaidi na kuruhusu watu zaidi wawe na nafasi ya kushiriki katika "Kumbukumbu za Urafiki wa China na Tanzania" Shindano la Uandishi wa Insha, Ubalozi wa China nchini Tanzania, baada ya kushauriana na waandaji wengine wa Shindano hilo, umeamua kuongeza tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kuwa Mei 15, 2019. Washiriki wenye uwezo wanakaribishwa kuwasilisha insha zao kabla ya tarehe ya mwisho. Tumefanya marekebisho kwa mahitaji ya insha zinazoshiriki. Mahitaji mapya ni kama ifuatavyo:

 

1. Mwandishi anapaswa kuwa raia wa China au wa Tanzania.

2.  Insha inatakiwa kuongelea hadithi moja au kadhaa zinazohusiana na urafiki wa China na Tanzania.

3. Insha zinapaswa kuandikwa kwa Kichina, Kiswahili au Kiingereza.

4. Urefu wa insha lazima uwe chini ya au takribani maneno 2,000 ya Kichina au maneno 2,000 ya Kiswahili au Kiingereza.

5.  Kila mshiriki atawasilisha kazi moja tu na picha 3 au video moja zikiambatanishwa. Ukubwa wa picha haipaswi kuzidi MB 5, na video haipaswi kuzidi dakika 2. Picha na video zinapaswa kuendana na hadithi zilizopo katika insha na kutumwa kwa kutenganishwa na insha.

6. Insha zote zinapaswa kuwa halisi, ambazo hazijachapishwa kabla. Kamwe haitakiwi kudurufu.

7. Insha zote zinapaswa kuwasilishwa katika muundo wa 'WORD', na kichwa cha habari, ujumbe, na wasifu mfupi wa mwandishi. Wasifu wa mwandishi haupaswi kuzidi maneno 200 ya Kichina au Kiswahili, Kiingereza. Inapaswa kujumuisha taarifa kama vile jina la mwandishi, ushirika, tarehe ya kuzaliwa, anwani ya posta, anwani ya barua pepe na nambari ya simu ya mkononi. Wasifu wa mwandishi unapaswa kuwekwa chini ya ujumbe katika aya tofauti.

8. Ukubwa na mfumo wa herufi katika insha lazima iwe: "Times New Roman, 15, "iliyo fifizwa " kwa kichwa cha habari; "Times New Roman, 13" kwa ujumbe; "Times New Roman, 12" kwa wasifu wa mwandishi. Lazima kuwe na nafasi moja kati ya mtari na mstari.

9. Washiriki wote wanapaswa kutuma kazi zao kupitia barua pepe tanzania55zw@gmail.com, na kichwa cha barua pepe kinapaswa kuwa "Shindano la Uandishi wa Insha + Jina la Mwandishi + Jina la Taasisi ya Mwandishi".

 

Waandaaji wa shindano wataunda jopo litakalohusisha wanadiplomasia, wasomi, waandishi wa habari na watu maarufu kuchagua insha bora na kuwapa tuzo. Insha zilizoshiriki zitagawanywa katika makundi mawili au matatu kutokana na lugha waliyotumia. Washindi wa kwanza, wa pili na wa tatu watazawadiwa vyeti vya heshima na bonasi ya Tsh. 300,000 / -, Tsh. 200,000 / - na Tsh. 100,000 / - kwa mtiririko huo. Tutachapisha insha bora katika tovuti ya Ubalozi, Wechat na Facebook akaunti ya Ubalozi, The Oriental Post, Daily News, Habari Leo na ikiwezekana katika kitabu kulingana na mazingira. 

                         

                          

                          Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China

                                 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

Suggset To Friend:   
Print