Mwanzo > Rolling News Report
Hotuba ya MHE. Balozi LU Youqing Katika "Sikukuu ya Spring yenye Furaha" ya Mwaka 2015
2015-02-16 19:38

Hotuba ya MHE. Balozi LU Youqing Katika “Sikukuu ya Spring yenye Furaha” ya Mwaka 2015

2015.2.18

MHE. Bernard Membe, Mwakilishi wa Rais Kikwete, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

MHE. Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi,

MHE. Dkt.Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,

Mabibi na Mabwana:

Habari za jioni! Karibuni katika Sherehe ya “Sikukuu ya Spring yenye Furaha”. Mwaka Mpya wa Kichina unakuja hivi karibuni, kwa niaba ya Ubalozi wa China nchini Tanzania, nawatakia Wachina nchini Tanzania, marafiki wenzangu wa Tanzania Heri ya Mwaka Mpya na Kila la Heri!

Sikukuu ya Spring ni Mwaka Mpya wa Kichina, ni sikukuu ya jadi muhimu kabisa nchini China. Sisi Wachina tumeshasherehekea sikukuu hii kwa zaidi ya miaka 4000. Sikukuu ya Spring inamaanisha kwamba majira ya spring yatakuja haraka, na maumbele yote yatakuwa na uhai tena. Inaonyesha furaha, heri, amani na maelewano. Sherehe ya “Sikukuu ya Spring”, kama alama ya kufahamu utamaduni wa China, imeshafanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka 6, na inapendeza sana na watu wa Tanzania, ni mfano mmoja mzuri sana wa ushirikiano baina ya China na Tanzania katika sekta ya utamaduni.

Mabibi na Mabwana,

Sherehe ya “Sikukuu ya Spring” ya mwaka huu ni sherehe yenye vipengele vipya. Ukilinganisha na sherehe za zamani, sherehe ya mwaka huu, muda ya kusherehekea imeongezeka, sehemu inapofanyika sherehe imeongezeka, idadi ya watu wanaohudhuria imeongezeka, na tamthiliya zinapendeza zaidi. Hivi karibuni, tumefanikiwa kufanya sherehe kubwa katika mikoa wa Dodoma, Arusha na Mwanza. Kipengele kimoja maalumu sana ni kwamba, mwaka huu, sisi hatualiki timu maalumu kutoka China kuja hapa Tanzania kufanya tamthiliya. Tamthiliya zote zinaandikwa, zinaongelewa na zinafanywa na watu wa China nchini Tanzania na marafiki wenzangu wa Tanzania. Wananchi wa nchi hizi mbili wameungana mikono kwa lengo moja kwa pamoja, kufanya mazoezi usiku kucha. Tunaamini kwamba ninyi nyote mtatazama siyo thamiliya nzuri sana tu, bali pia mnaweza kutazama urafiki unaoonyeshwa na thamiliya baina ya China na Tanzania. Nataka kutoa shukrani zangu za dhati kwa uungaji mkono wa serikali ya Tanzania, pia nawashukuru sana wachezaji na wafanyakazi wote wa China na wa Tanzania katika sherehe hii.

Mabibi na Mabwana,

Uhusiano wa China na Tanzania sasa uko katika kipindi kizuri cha juu. Mwaka 2014 uliopita ni miaka 50 ya uhusiano wa diplomasia baina ya China na Tanzania, kwa nusu karne, nchi hizi mbili zinasaidiana, na urafiki baina ya nchi hizi mbili umepata maendeleo makubwa sana. Mwezi wa 10, mwaka 2014, Rais Kikwete alifanikiwa kufanya ziara rasmi nchini China, viongozi wa nchi hizi mbili wameamua kukuza uhusiano wa ushirikiano na wa kiuenzi kwa pande zote kwa njia ya kunufaishana, kujenga uhusiano wa China na Tanzania uwe mfano wa uhusiano kati ya China na Bara Afrika. Tunaweza kujigamba kwamba uhusiano wa China na Tanzania umeingia maeneo yote ya maendeleo ya siasa na uchumi wa Tanzania. Takwimu kutoka Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania imeonyesha kwamba, China inachukua nafasi ya pili katika uwekezaji wa nchi za nje nchini Tanzania. Hadi mwisho wa mwaka 2013, idadi ya kiasi cha uwekezaji wa China nchini Tanzania ni zaidi ya Dola bilioni 3.15. Makampuni ya Kichina yamewapa Watanzania nafasi za ajira zaidi ya laki 1.5. Vilevile, China inashika nafasi ya kwanza katika sekta ya biashara na nchi za nje ya Tanzania. Idadi ya kiasi cha biashara kati ya China na Tanzania imefikia Dola Bilioni 4, Watanzania zaidi ya laki 4 wanafanya kazi za kibiashara na China. Kwa msaada wa mkopo nafuu wa Dola Bilino 1.2 za Marekani, Mradi wa Bomba la Gesi la Mtwara utakamilika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo Maalumu la Uchumi, kama Rais Kikwete alivyosema, ni mradi wa kwanza kwa Tanzania, utaanza mwaka huu vilevile. Miradi hii mikubwa itasaidia kutatua matatizo ya maendeleo ya Tanzania, kuchepuka kwa maendeleo ya viwanda, na vilevile kuwapa Watanzania ajira nyingi na mapato mengi kwa serikali. Kwa hivyo, itaipa Tanzania nguvu ya maendeleo ya siasa na uchumi, na kuongeza nguvu kwa urafiki baina ya China na Tanzania.

Mabibi na Mabwana,

Katika sherehe hii, maofisa wote na familia zetu tutaimba wimbo mmoja kwa Kichina na Kiswahili unaoitwa <Tupige Jahazi Iende Mbali>. Wimbo huu unasema kwamba Umoja ni Nguvu, kama tunataka kutimiza ndoto zetu, ni lazima tuungane mikono na tushirikiane kwa pamoja! Na vilevile, maendeleo ya China na Tanzania, hasa maendeleo imara ya uhusiano wa China na Tanzania, yanataka ushirikiano wa wananchi wa nchi hizi mbili. Katika Mwaka Mpya, naomba tushirikiane na tusaidiane, ili kuzidisha uhusiano wa China na Tanzania kupata matunda mazuri mengi zaidi!

Mwishoni, kwa moyo wa dhati, nawatakia Heri ya Mwaka Mpya, na Kila la Heri ya Mwaka wa Mbuzi!

Asanteni kwa kunisikiliza.

Suggset To Friend:   
Print